ETETA | Home juu

Kuhusu ETETA

Mpango huu wa ETETA umeanzia katika Sekretariati ya Mkoa wa Morogoro, Sehemu ya Elimu mwaka 2018. Lengo kuu ni kutimiza utekelezaji wa mpango mkakati wa Mkoa wa mwaka 2018 hadi 2022 ulioazimia kutumia TEHAMA katika kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii ikiwemo kuinua kiwango cha Elimu kufikia Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati vitakavyoleta ustawi wa maisha ya wananchi wote. Serikali kwa dhati imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda na Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

DIRA

ETETA itakuwa na mifumo itakayotoa Elimu kwa njia ya TEHAMA nchi nzima na kwa kiwango cha juu ikianzia Mkoani Morogoro.

DHIMA

Mpango wa ETETA utasaidia kutoa Elimu kwa kiwango cha juu kwa walimu na wanafunzi shuleni ili kuongeza ufaulu na ufanisi katika Elimu ya Mkoa wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla

LENGO KUU

Kuufanya Mkoa wa Morogoro uwe na uwezo wa kutoa Elimu kwa njia za Kidigitali ifikapo mwaka 2022.


Wahisani

  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani