ETETA | Home juu

MSICHANA JITAMBUE

“MSICHANA JITAMBUE” ni kampeni inayosimamiwa na usimamizi wa kiongozi wa timu Vicky D. Sengela na daktari anayewakilisha masuala ya kiafya Neema Mwakifuna.

Kuelimisha wasichana wa shule juu ya umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi na taulo za usafi(PEDI),

Na kuwasihi wasichana wajitambue katika masuala mbalimbali yanayo wakabili ilikufikia ndoto zao kimasomo,

“Kwa pamoja tunaweza Kuwa suluhisho la shida za jamii yetu na jibu la kilio cha kizazi chetu."


Habari Mpya Kuhusu Shughuli Zetu

Imewekwa 2020-12-02

Tafakari; SIKU YA KIMATAIFA YA UKIMWI DUNIANI

Jana Desemba 01, 2020 ilikuwa siku ya kimataifa ya UKIMWI duniani. Siku hii inatupa nafasi ya kutafakari juu ya janga hili ambalo bado limeigubika dunia huku likiendelea kudhoofisha afya za watu na hata kusitisha maisha yao. Ni ugonjwa ambao bado wanasayansi hawajapata tiba yake. Huwa ninapenda nisikiapo mtu akijisemea  “Hata kama sina pesa, nikiwa na afya nzuri ninamshukuru Mungu”.

Angalau sasa kila mtu anaelewa nini maana ya UKIMWI. Hiki ni kifupisho cha ‘Upungufu wa Kinga Mwililini’. Huu ni ugonjwa unaosababisha mwili kukosa uwezo wa kupambana na vimelea vya magonjwa kutokana na kinga yake kushuka. Hivyo mgonjwa anakuwa na hatari ya kushambuliwa na magonjwa mengine hata madogo madogo kwa urahisi.

Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kwamba takwimu zinaonesha ongezeko la maambukizi mapya ukimwi kwa vijana walio na umri mdogo kati ya miaka 14-25 ambao ndiyo nguvu kazi ya familia na taifa kwa ujumla. Vijana wengi walio katika umri wanakuwa bado ni wanafunzi wa shule au chuo wakijiandaa kuingia katika soko la ajira.

Mtu anapougua ugonjwa wa UKIMWI au hata ugonjwa mwingine utakaomsababishia kushindwa kushiriki vyema shughuli zake binafsi au za kuajiriwa anakuwa katika hatari ya kupoteza kipato chake huku akilazimika kutumia pesa nyingi kwenye matibabu.

Athari kubwa ya kuugua muda mrefu ukiwa hujiwezi, inapelekea ndugu wa karibu yako nao kuacha shughuri zao ili kukuhudumia wewe. Hivyo, unaweza kukuta katika familia moja jumla ya watu watatu au zaidi hawafanyi tena shughuli zao kikamilifu kwasababu ya kumsaidia mgonjwa mmoja asiyejiweza.

Katika hali kama hiyo kama familia ilikuwa maskini itazidi kuwa fukara zaidi kwasababu ya mtu mmoja anayeugua.

Kwa upande mwingine serikali inapata athari kubwa sana kutokana na magonjwa kama haya. Kama ni mwajiriwa anaweza akapunguza kasi ya uwajibikaji na uzalishaji; pia serikali inaweza kukosa mapato ya kodi kama mtu atashindwa kufanya kazi kabisa. Kumbuka serikali ni mimi na wewe, hivyo serikali yenye wagonjwa wengi kama hawa haiwezi kupiga hatua ya kimaendeleo; nayo itakuwa kama iko taabani wodini.

Zaidi ni kwamba serikali inalazimika kutumia gharama kubwa kutoa matibabu ya bure kwa wenye UKIMWI na wakati mwingine dawa hizo zinanunuliwa kwa mikopo inayolipwa na kodi za wananchi wengine. UKIMWI unaepukika kwa kufuata kanuni zinazoelezwa na wataalamu wa afya.

Hebu fikiria; Kama serikali inatakiwa iwatibu bure watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee, kwanini wewe kijana mwenye nguvu usiukimbie UKIMWI ili bajeti iliyopo iwatosheleze makundi hayo mengine tu?

Tafakari, chukua hatua!

Imeandaliwa na;

Mwl. Wilson Anatory

Kilakala Sekondari

Imewekwa 2019-09-13

Msichana Jitambue

Daktari Neema Mwakifuna Mdau wa MSICHANA JITAMBUE akitoa elimu ya afya kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kipera akielimisha wanafunzi wa kike kuhusu matumizi sahihi ya taulo za kike(PEDI)

Imewekwa 2019-09-13

Msichana jitambue

Mratibu wa kampeni ya MSICHANA JITAMBUE Vicky D.Sengela akiwa na Daktari Neema Mwakifuna Wakimkabidhi Taulo za kike(PEDI) Mkuu wa shule ya sekondari kipera  iliyoko wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro.

Imewekwa 2019-09-13

Msichana jitambue

Mratibu wa kampeni ya MSICHANA JITAMBUE  Vick D. Sengela katika shule ya sekondari kipera ni baada ya kuwakabidhi wanafunzi wa kike taulo za kike(PEDI)akiwa pamoja na wadau wa  kampeni hiyo pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari kipera iliyoko wilayani mvomero Mkoa wa Morogoro.

Imewekwa 2019-09-13

Msichana jitambue

Wadau wa Kampeni ya MSICHANA JITAMBUE wakiongozwa na Mratibu wa kampeni hiyo Vicky D.Sengela katika shule ya sekondari kipera wakitoa Elimu juu ya Masuala mbalimbali ya kiafya Na kutoa msaada wa taulo zakike(PEDI) Kwa wanafunzi wa kike  wa shule hiyo.

Imewekwa 2019-09-13

Msichana jitambue

Wanafunzi wakike shule ya sekondari kipera wakiwa katika furaha kutokana na ujio wa Mratibu wa kampeni ya MSICHANA JITAMBUE Vick D. Sengela ulio pelekea kupewa taulo za kike(PEDI) ili kuwalinda katika masuala ya kiafya na kitaaluma kwa ujumla. 

Wahisani

  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani