
Elizabeth ngaiza katika utekelezaji wa kampeni yake ya NIACHE NISOME KWANZA
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Bi Elizabeth ngaiza akiwa katika majukumu yake ya kutekeleza kampeni ya NIACHE NISOME KWANZA
"NIACHE NISOME KWANZA" ni kampeni Inayo endeshwa na kikundi kinacho julikana kama Magufuli Tubebe, Ni kikundi kinachoendesha kampeni ya kuzuia mimba za utotoni, Kilichozinduliwa Tarehe 29/3/2019 Na Mratibu wa Kikundi hiki Bi.Elizabeth Ngaiza Mengi katika viwanja vya shule ya msingi Lupilo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Kampeni hii inalenga kuhakikisha watoto wetu wa kike wanapata nafasi ya kutimiza ndoto zao, wanaume wenye tabia za kuwadanganya mabinti na kuwapa ujauzito wakemewe katika Nchi hii.
Tuwaache watoto wasome kwanza "NIACHE NISOME KWANZA". Kupitia Kampeni hii tuliyoizindua tuna hakikisha watuhumiwa wa kesi hizi wanafikishwa mahakamani
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Bi Elizabeth ngaiza akiwa katika majukumu yake ya kutekeleza kampeni ya NIACHE NISOME KWANZA
Watanzania na jamii nzima ni napenda kuwaomba tushirikiane kuwalinda watoto wa kike ili watimize ndoto zao, mimba za utotoni limekuwa janga la kitaifa lakini ninaamini kuwa inawezekana endapo serikali ikiamua ,mbona iliamua viroba visiwepo, mbona Madawa ya kulevya hayapo? Serikali ni wapi inashindwa ktk kuwalinda watoto?Tuungane pamoja NIACHE NISOME KWANZA
Nashukuru Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kilakala iliyopo mkoani morogoro kwa ushirikiano wako kwetu, kuonyesha jinsi suala la mimba za utotoni Morogoro linavyorudisha nyuma maendeleo ya Taifa,
Muuendelezo wa kampeni ya niache NISOME KWANZA inayoendele Wilaya ya Ulanga katika Mkoa wa Morogoro
Uzinduzi wa kampeni ya NISOME KWANZA iliyozinduliwa mkoani morogoro na Afisa Elimu Mkoa Eng. Joyce Baravuga, mama mlezi wa shule za msingi na sekondari.