Utekelezaji Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa 2015-2030
Lengo la tisa la mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa, linalenga kukuza uelewa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kusaidia kushughulikia changamoto kubwa za duniani kama vile kujenga ajira na kuwa na nguvu zaidi ya Nishati na Matumizi bora ya mawasiliano ya Mtandao
Kuongeza Idadi ya Watumiai wa TEHAMA Tanzania
Kutokana na Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia mitandao na Matumizi ya TEHAMA (ICT Index), kwenye ripoti yake ya mwaka 2017 inaonyesha kuwa nchi ya Tanzania ni ya 164 kati ya nchi 169 Duniani katika matumizi ya TEHEMA. Hii inaonyesha tunahitataji kuongeza idadi ya watumiaji wa TEHAMA katika Shughuli za Kila Siku za kuleta Maendeleo.