ETETA | Home juu

TAARIFA FUPI YA UZINDUZI WA MFUMO WA KUFUNDISHIA KIDIGITALI MASHULENI UITWAO T-ESCHOOLS ULIOTENGENEZWA NA TAASISI YA APPS AND GIRLS, NLAB INNOVATION ACADEMY NA KUWEZESHWA NA TIGO TANZANIA

( Kutoka kulia waliosimama ni Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Eng. Joyce Baravuga akiongea na Mwanzilishi wa APPS AND GIRLS ndugu Carolyne Ekyarisiima pamoja na Mkurugenzi wa chuo cha Nlab Innovation Academy ndugu Wilhelm Capsr Oddo wakati wa uzinduzi wa programu ya Elimu Mtandao Teschool – Mkoani Morogoro)

 

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imeendeleza dhamira yake katika kusaidia wanafunzi katika

nyanja ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kupitia taasisi ya Apps and Girls

pamoja na taasisi ya Nlab Innovation Academy.

 

Apps and Girls na Nlab Innovation Academy wametengeneza mfumo wa kidigitali unaojulikana

na kama Teschool ambao unatoa fursa ya kujifunza kwa wanafunzi katika maeneo ya vijijini na

mijini kote Tanzania. Mfumo huu unalenga kuwaunganisha wanafunzi, wazazi na walimu

pamoja na kuboresha fursa ya elimu kwa wasomaji wa majumbani.

 

Uzinduzi wa programu hii umefanywa tarehe 28 agosti 2020 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro

Loata Ole Sanare katika shule ya Sekondari Morogoro na kuhudhuriwa na Katibu Tawala wa

Mkoa wa Morogoro Eng.Emmanuel L.M. kalobelo pamoja na Maafisa mbalimbali wa serikalini

Hii ni kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Apps and Girls, Nlab Innovation Academy na

Idara ya Elimu Mkoa wa Morogoro katika kuchochea matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji

na ujifunzaji shuleni.

 

Ikumbukwe kuwa Idara ya Elimu Mkoa wa Morogoro inatekeleza mpango wa Elimu Kwa

TEHAMA (ETETA) ulioanza tangu mwaka 2018 ukiwa na lengo la kuufanya Mkoa huo kuwa

wa kidigitali ifikapo mwaka 2022.

 

“Mfumo uliotengenezwa na Apps and Girls pamoja na Nlab utawawezesha wanafunzi kuhudhuria vipindi mtandaoni vikifundishwa na walimu wa somo husika, pia itawapatia wanafunzi nafasi ya kuuliza maswali na kufanya majaribio. Vipindi hivyo vitakuwa vinarekodiwa hivyo kumuwezesha mwanafunzi kurejea masomo wakati wowote’’ alisema Bwana Wilhelm Caspar Oddo, Mkurugenzi wa Nlab Innovation Academy.

 

Vipindi vilivyorekodiwa pia vitapatikana kwa njia ya ujumbe mfupi unaowezeshwa na kampuni ya Tigo Kupitia utekelezaji huu tunatarajia kufikia shule za msingi na sekondari kote Tanzania, lakini kwa awamu hii ya kwanza hapa Morogoro tunatarajia kuwa na shule 150 za sekondari na 400 za msingi ambazo zitakuwa hai katika mfumo wetu wa kidigitali.

 

Uzinduzi huu umetanguliwa na mafunzo ya walimu wa Morogoro ambao walijengewa uwezo wa

namna ya kutumia mfumo huu wa kidigitali na kupewa rasilimali kazi zitakazoweza kuwasaidia

kutumia kikamilifu mfumo huu na kusaidia wanafunzi watakaotumia mfumo huu.

Taarifa hii imetolewa na ndugu Wilhelm Caspar Oddo, Mkurugenzi wa Nlab Innovation Academy, na kuletwa kwako na;

Wilson Anatory

ETETA TV - MOROGORO

Wahisani

  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani