ETETA | Home juu

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - Rc Sanare

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Eresto Ole Sanare amesema wajibu wa kwanza kwa mtumishi wa Umma ni kumtumikia mwananchi, kumheshimu na kuhakikisha anamletea maendeleo yanayotarajiwa kwa lengo la kumuondolea changamoto zinazomkabili.
Mhe. Sanare ameyasema hayo Septemba 25 Mwaka huu wakati  akizungumza na watumishi wanaofanya kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha rasmi kwa watumishi hao na kuweka mikakati ya namna ya kufanya kazi kwa lengo la kuwaleeta maendeleo wananchi wa Mkoa huo na watanzania wote kwa jumla.

Akiweka wazi msimamo wake kwa watumishi hao Ore Sanare amesema wajibu wao wa kwanza  uwe ni kuwahudumia wananchi kwa kuwa hao ndio mabosi wao. “…mtumishi yeyote akitaka kumheshimu Rais amheshimu kwanza mwananchi kwa kuwa ni wajibu wake kumtumikia na ndiye bosi wake” alisema Ore Sanare..Aidha, Mhe. Ore Sanare amesema hayupo tayari kufanya kazi na mtumishi asiyewajibika na kama yupo ni vema kuchukua uamuzi mwingine mapema. “Sitokuwa tayari kufanya kazi na mtumishi yeyote asiyejituma , kama unajiona huwezi kufanya kazi ipasavyo ni vyema ukachukua kilicho chako na kuwapisha wengine…” alisisitiza.
Sambamba na hilo amewataka watumishi hao kusaidiana katika kutafuta kiini cha tatizo linalochelewesha maendeleo  katika Mkoa wa Morogoro  huku akiwataka wataalamu kuwasilisha kwa wakati taarifa muhimu zinazotakiwa zimfikie ili zisaidie kutoa ufumbuzi kwa changamoto zilizopo.

 Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Masasi Kalobelo ambaye naye aliripoti siku moja na Mkuu huyo wa Mkoa huo amewataka watumishi kuwajibika na kufanya  kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya iliyotolewa na Serikali.Amesema ni wakati sasa watumishi wote wa Ofisi hiyo kubadilika kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kufanya kazi kwa ufanisi  ili kuendana na mabadiliko yenye lengo la kufanya mageuzi katika Mkoa huo hususan katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.


Katika kikao hicho pia watumishi wanaofanya kazi  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa maana ya makao Makuu walipata fursa ya kutoa changamoto zinazowakabili katika shughuli zao ambapo Katibu Tawala wa Mkoa huo alizipokea na kwamba atazifanyia kazi.
Hicho ni kikao cha kwanza kabisa tangu Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wake kuwasili Ofisini hapo Septemba 23 mwaka huu.

Video; Sitofanya kazi na mtumishi asiyejituma - RC Sanare

Wahisani

  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani