ETETA | Home juu

China kusaidia wakulima teknolojia za mazao ili kulima kwa tija

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA)pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China katika kuhakikisha wakulima wanaingia kwenye mapinduzi ya kilimo cha kisasa na kibiashara wameanza kusaidia teknolojia za mazao kwa wakulima hao ili waweze kulima kwa tija.

 

Kaimu makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Peter Gilla, alizungumza hayo jana wakati mafunzo elekezi yanayohusu teknolojia Jumuishi za kilimo kwa maafisa Ugani wa vijiji, na wilaya  wa mikoa ya Morogoro na Dodoma, yaliyoandaliwa na chuo kikuu cha Kilimo cha China na SUA kupitia wizara zake chini ya mradi wa kuongeza tija kwenye zao la Mahindi.

 

Profesa Gilla alisema kwa muda mrefu vyuo hivyo vimekuwa vikishirikiana katika masuala mbalimbali ya kilimo hasa cha biashara,na kwamba katika ushirikiano huo wameweza kuleta tija kwa wananchi kupitia mpango wa maendeleo wa Taifa(ESDP ll) na kumekuwa na kituo maalumu cha ushirikiano kwa ajili ya kutoa mafunzo.

 

Aidha vyuo hivyo pamoja na kusaidia teknolojia hizo lengo ni kuwafikia vijana wakulima ili waweze kutoka katika kilimo cha Mazoea na kulima kisasa na kuleta mageuzi makubwa katika kilimo.

 

Alisema ili kufanya hivyo vijana lazima waweze kushirikishwa katika kila hatua na unapozungumzia mapinduzi uwezi kukwepa kuongeza uzalishaji wa mazao ili kuwasaidia wakulima kwa ukaribu zaidi.

 

“Tayari wenzetu wachina wamesonga mbele zaidi kwenye mbambo ya teknolojia hasa hizo ndogo, hivyo kupitia kituo hiki maprofesa wa Sua na China wanachukua teknolojia hizo ambazo ni rafiki kwa wananchi na kuzifanyia uwahakiki ili kuweza kuwafikishia wakulima na zitaongeza uzalishaji.

 

Alisema teknolojia ndogo zinakwenda na kusaidia kuweza kuongeza kipato na kukua kiuchumi na mpaka sasa vijiji sita vimefikiwa na kwamba vinaendelea kufika mbali na baadhi ya teknolojia zinachukuliwa na kuendelea kuwaelekeza wakulima hao,”alisema.

 

Profesa Gilla alitaja teknolojia zitakazowanufaisha wakulima hao ni pamoja na zile za masuala ya Umwagiliaji, matumizi ya mbolea, na matumizi madogo ya Maji kwani suala la maji bado limekuwa changamoto kwenye maeneo mengi hivyo teknolojia itasaidia kubana matumizi madogo na nia ni kuwafikia walengwa hasa wale wa vijijini.

 

Mratibu wa mradi wa kuongeza tija kwenye zao la Mahindi toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Evans Gambishi alisema mradi huo ulinza tangu 2011 wilayani Kilosa, Gairo, Mvomero, Ulanga Malinyi na Kilimbero na baada ya maendele kuongekana kuleta tifa  ziliongezeka wilaya nyingine za Morogoro na Dodoma lengo likiwa ni kuzalisha zao la Mahindi kwa kutumia teknolojia rahisi na kufuata mbinu bora za kilimo.

 

Gambishi alisema baada ya mafanikio yaliyopatikana wakulima waliongeza uzalishaji kutoka gunia tatu hadi kufikia gunia 15 na kuongeza kipato na uchumi kukua ikiwa ni pamoja na kubadilisha maisha yao.

 

Alisema Mradi huo unafanyika kuwafundisha mabwana na mabibi shamba ambao watatumika zaidi kuwafundisha wakulima katika maeneo yao, na kwamba mbinu na teknolojia mpya zitasaidia uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi kwani zao hilo ni namba moja la chakula likifatiwa na Mpunga.

 

Naye mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara  Yang Lijuu akaeleza kuwa ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na China hasa katika Nyanja za kilimo umendelea kukuza na kuleta tija kwa wananchi katika suala zima la kilimo.

 

Lijuu alisema china imekuwa bora katika suala la Kilimo kutokana na wananchi wake kuonyesha utayari wa kufanya kazi hiyo ya kilimo hivyo ni vyema wananchi nchini hasa wale wa vijijini wakawa tayari pindi wanapopata miradi kama hiyo ambayo ni hakika itaweza kuleta faida kwa mtu mmoja na vikundi.

Wahisani

  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani
  • Wahisani