ETETA | Home juu

Habari na Matukio

Imewekwa Tarehe 2020-01-28

UTALII WA NDANI NI MUHIMU – LOATA SANARE



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Kamishina Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Mashariki Stelia Ndaga inayojumuisha Hifadhi za Taifa za Mikumi, Milima ya Udzungwa, Hifadhi ya Nyerere na Saadani kuhakikisha wanahamasisha wananchi Utalii wa Ndani ili kuongeza pato kwa Serikali pamoja na wao kufaidi kuona rasilimali zilizoko katika Hifadhi hizo.

Ole Sanare ametoa agizo hili Januari 27 mwaka huu akiwa katika Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni siku yake ya kwanza ya Ziara ya siku tatu ya kutembelea Hifadhi zote za Taifa zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Morogoro.

Soma Zaidi

Imewekwa Tarehe 2019-12-06

Magereza Yarejesha Eneo kwa Wananchi Ifakara, RC akumbusha wazazi kuwapeleka watoto shule

Serikali kupitia Jeshi la Magereza Nchini imerejesha eneo la hekari 50 kwa wananchi wa kitongoji cha Nakafuru, kijiji cha Milola kata ya Kibaoni Halmashauri ya Mji wa Ifakara lililokuwa linamilikiwa na Jeshi hilo tangu mwaka 2010 kwa lengo la kujenga Magereza ya Mahabusu.

Akifikisha Ujumbe wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kurejesha eneo hilo kwa wananchi, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Faustin Kasike amesema eneo hilo kwa sasa ni la wananchi wa kijiji hicho wanaostahili na kuagiza pasitokee mgogoro wowote.

“Natambua sote tunafahamu kwamba Jeshi la Magereza lilkuwa na mpango wa kujenga Magereza katika Wilaya hii ya Kilombero katika Eneo hili la Milola, lakini sasa Mhe. Rais ameamua kurejesha eneo hili kwenu wananchi ili mliendeleze”, alisema Kasike.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare pamoja na kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali wananchi wake, ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi walionyang’anywa maeneo yao ndio wapatiwe haki yao.

Aidha Sanare hakusita kuwakumbusha wazazi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2020 kuhakikisha wanawapeleka shuleni pindi shule zinapofunguliwa kwa kuwa elimu ni haki yao ya msingi.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo James Ihunyo amesema Halmashauri yake itahakikisha inasimamia vyema maeneo hayo ili wananchi wenye haki warejeshewe haki yao.

Hata hivyo wananchi wa Halmashauri hiyo pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuwarejeshea eneo lao, wameiomba kuangalia uwezekano wa kuwalipa fidia kwani hawakuwa wakifanya shughuri yoyote kwa karibu kipindi cha miaka tisa huku baadhi ya nyumba zilizojengwa awali zikiharibika.

Kwa kipindi cha karibu miaka tisa wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakidai kurejeshewa eneo hilo ambalo awali walikuwa wakilitumia kwa shughuli za makazi kabla ya Jeshi la Magereza kulichukua kwa lengo la kujenga Magereza.

                                                                           MWISHO

Soma Zaidi
Imewekwa Tarehe 2019-10-24

RC Sanare agiza Sokoine Memorial High School kupokea wanafunzi.

RC Sanare agiza Sokoine Memorial High School kupokea wanafunzi.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare amewaagiza Afisa Elimu wa Mkoa huo na Viongozi wa Wilaya ya Mvomero na Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha Sekondari ya Sokoine Memorial High School iliyopo Wilayani humo inapokea wanafunzi kwa ajili ya kuanza masomo mwaka huu bila kukosa.


Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo hilo leo Oktoba 24 alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa Ujenzi wa mradi huo pamoja na majengo ya Mama na Mtoto yanayojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero.


“miaka saba mradi unajengwa mmoja, sasa naomba tubadilishe staili, Mkurugenzi, lazima sasa hivi tuwachukue watoto sasa hawa wanaokuja, hakuna tena mjadala …….tuanze tufanye finishing (umaliziaji) wa majengo yale ya muhimu…tuanze sasa kuchukua watoto” amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.


Ole Sanare amesema sio busara kusubiri fedha kiasi cha shilingi Bilioni 12 zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa majengo hayo ndipo tuanze kuwapokea wanafunzi hao kwa ajili ya kuanza masomo bali fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni mia moja zitumike kumalizia majengo yaliyopo mwishoni kumalizika ili wanafunzi waanze masomo mwaka huu.


Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi wa Wilaya ya Mvomero kumpa ushirikiano ili kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi Wilayani humo huku akiwaahidi kurudi tena ili kukaa nao na kujadili changamoto ya Migogoro ya Ardhi baina ya wakulima na wafugaji inayoendelea kujitokeza ili kuipatia ufumbuzi wa kudumu.


Hata hivyo amewataka wananchi wa Halmashauri hiyo kuishi kama ndugu na kujikita kwenye masuala ya maendeleo ikiwemo suala la Elimu badala ya kuendekeza Migogoro isiyo na tija kwao.


Awali akitembelea majengo yanayojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero yatakayotoa huduma ya mama na Mtoto, Mhe. Ole Sanare aliwapongeza Viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia fedha za Serikali zaidi ya shilingi 500 Mil.


Amesema katika mradi huo sio tu unakamilika kwa wakati lakini pia kwa kiwango bora kinachoendana na fedha zilizotolewa na Serikali.


Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl. Mohamed Utali pamoja na kupokea maagizo ya Mkuu huyo wa Mkoa alieleza sababu inayopelekea kiasi cha shilingi milioni mia moja kinachotakiwa kutumika katika kujenga njia ya kupita wagonjwa kutoka jengo moja hadi jingine (Walk way).


Akitoa taarifa ya ujenzi wa Sekondanri ya Sokoine Memorial High School, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mvomero Florent Kyombo amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa mradi huo awali ulitengewa fedha Bil. 12 lakini baada ya uamuzi wa Serikali wa Kutumia Force akaunti, mradi huo sasa utakamilisha ujenzi wake kwa shilingi Bil. 7 pekee.


MWISHO

Soma Zaidi
Imewekwa Tarehe 2019-09-19

China kusaidia wakulima teknolojia za mazao ili kulima kwa tija

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA)pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China katika kuhakikisha wakulima wanaingia kwenye mapinduzi ya kilimo cha kisasa na kibiashara wameanza kusaidia teknolojia za mazao kwa wakulima hao ili waweze kulima kwa tija.

 

Kaimu makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Peter Gilla, alizungumza hayo jana wakati mafunzo elekezi yanayohusu teknolojia Jumuishi za kilimo kwa maafisa Ugani wa vijiji, na wilaya  wa mikoa ya Morogoro na Dodoma, yaliyoandaliwa na chuo kikuu cha Kilimo cha China na SUA kupitia wizara zake chini ya mradi wa kuongeza tija kwenye zao la Mahindi.

 

Profesa Gilla alisema kwa muda mrefu vyuo hivyo vimekuwa vikishirikiana katika masuala mbalimbali ya kilimo hasa cha biashara,na kwamba katika ushirikiano huo wameweza kuleta tija kwa wananchi kupitia mpango wa maendeleo wa Taifa(ESDP ll) na kumekuwa na kituo maalumu cha ushirikiano kwa ajili ya kutoa mafunzo.

 

Aidha vyuo hivyo pamoja na kusaidia teknolojia hizo lengo ni kuwafikia vijana wakulima ili waweze kutoka katika kilimo cha Mazoea na kulima kisasa na kuleta mageuzi makubwa katika kilimo.

 

Alisema ili kufanya hivyo vijana lazima waweze kushirikishwa katika kila hatua na unapozungumzia mapinduzi uwezi kukwepa kuongeza uzalishaji wa mazao ili kuwasaidia wakulima kwa ukaribu zaidi.

 

“Tayari wenzetu wachina wamesonga mbele zaidi kwenye mbambo ya teknolojia hasa hizo ndogo, hivyo kupitia kituo hiki maprofesa wa Sua na China wanachukua teknolojia hizo ambazo ni rafiki kwa wananchi na kuzifanyia uwahakiki ili kuweza kuwafikishia wakulima na zitaongeza uzalishaji.

 

Alisema teknolojia ndogo zinakwenda na kusaidia kuweza kuongeza kipato na kukua kiuchumi na mpaka sasa vijiji sita vimefikiwa na kwamba vinaendelea kufika mbali na baadhi ya teknolojia zinachukuliwa na kuendelea kuwaelekeza wakulima hao,”alisema.

 

Profesa Gilla alitaja teknolojia zitakazowanufaisha wakulima hao ni pamoja na zile za masuala ya Umwagiliaji, matumizi ya mbolea, na matumizi madogo ya Maji kwani suala la maji bado limekuwa changamoto kwenye maeneo mengi hivyo teknolojia itasaidia kubana matumizi madogo na nia ni kuwafikia walengwa hasa wale wa vijijini.

 

Mratibu wa mradi wa kuongeza tija kwenye zao la Mahindi toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Evans Gambishi alisema mradi huo ulinza tangu 2011 wilayani Kilosa, Gairo, Mvomero, Ulanga Malinyi na Kilimbero na baada ya maendele kuongekana kuleta tifa  ziliongezeka wilaya nyingine za Morogoro na Dodoma lengo likiwa ni kuzalisha zao la Mahindi kwa kutumia teknolojia rahisi na kufuata mbinu bora za kilimo.

 

Gambishi alisema baada ya mafanikio yaliyopatikana wakulima waliongeza uzalishaji kutoka gunia tatu hadi kufikia gunia 15 na kuongeza kipato na uchumi kukua ikiwa ni pamoja na kubadilisha maisha yao.

 

Alisema Mradi huo unafanyika kuwafundisha mabwana na mabibi shamba ambao watatumika zaidi kuwafundisha wakulima katika maeneo yao, na kwamba mbinu na teknolojia mpya zitasaidia uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi kwani zao hilo ni namba moja la chakula likifatiwa na Mpunga.

 

Naye mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara  Yang Lijuu akaeleza kuwa ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na China hasa katika Nyanja za kilimo umendelea kukuza na kuleta tija kwa wananchi katika suala zima la kilimo.

 

Lijuu alisema china imekuwa bora katika suala la Kilimo kutokana na wananchi wake kuonyesha utayari wa kufanya kazi hiyo ya kilimo hivyo ni vyema wananchi nchini hasa wale wa vijijini wakawa tayari pindi wanapopata miradi kama hiyo ambayo ni hakika itaweza kuleta faida kwa mtu mmoja na vikundi.

Soma Zaidi
Imewekwa Tarehe 2019-09-26

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - Rc Sanare

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Eresto Ole Sanare amesema wajibu wa kwanza kwa mtumishi wa Umma ni kumtumikia mwananchi, kumheshimu na kuhakikisha anamletea maendeleo yanayotarajiwa kwa lengo la kumuondolea changamoto zinazomkabili.
Mhe. Sanare ameyasema hayo Septemba 25 Mwaka huu wakati  akizungumza na watumishi wanaofanya kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha rasmi kwa watumishi hao na kuweka mikakati ya namna ya kufanya kazi kwa lengo la kuwaleeta maendeleo wananchi wa Mkoa huo na watanzania wote kwa jumla.

Akiweka wazi msimamo wake kwa watumishi hao Ore Sanare amesema wajibu wao wa kwanza  uwe ni kuwahudumia wananchi kwa kuwa hao ndio mabosi wao. “…mtumishi yeyote akitaka kumheshimu Rais amheshimu kwanza mwananchi kwa kuwa ni wajibu wake kumtumikia na ndiye bosi wake” alisema Ore Sanare..Aidha, Mhe. Ore Sanare amesema hayupo tayari kufanya kazi na mtumishi asiyewajibika na kama yupo ni vema kuchukua uamuzi mwingine mapema. “Sitokuwa tayari kufanya kazi na mtumishi yeyote asiyejituma , kama unajiona huwezi kufanya kazi ipasavyo ni vyema ukachukua kilicho chako na kuwapisha wengine…” alisisitiza.
Sambamba na hilo amewataka watumishi hao kusaidiana katika kutafuta kiini cha tatizo linalochelewesha maendeleo  katika Mkoa wa Morogoro  huku akiwataka wataalamu kuwasilisha kwa wakati taarifa muhimu zinazotakiwa zimfikie ili zisaidie kutoa ufumbuzi kwa changamoto zilizopo.

 Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Masasi Kalobelo ambaye naye aliripoti siku moja na Mkuu huyo wa Mkoa huo amewataka watumishi kuwajibika na kufanya  kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya iliyotolewa na Serikali.Amesema ni wakati sasa watumishi wote wa Ofisi hiyo kubadilika kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kufanya kazi kwa ufanisi  ili kuendana na mabadiliko yenye lengo la kufanya mageuzi katika Mkoa huo hususan katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.


Katika kikao hicho pia watumishi wanaofanya kazi  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa maana ya makao Makuu walipata fursa ya kutoa changamoto zinazowakabili katika shughuli zao ambapo Katibu Tawala wa Mkoa huo alizipokea na kwamba atazifanyia kazi.
Hicho ni kikao cha kwanza kabisa tangu Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wake kuwasili Ofisini hapo Septemba 23 mwaka huu.

Video; Sitofanya kazi na mtumishi asiyejituma - RC Sanare

Soma Zaidi

Video

TAZAMA Jinsi Rais Ramaphosa alivyo tembelea eneo la Mazimbu,Morogoro
TAZAMA Jinsi Rais Ramaphosa alivyo tembelea eneo la Mazimbu,Morogoro
JPM AMWAMBIA POLEPOLE "SITAONGEZA HATA DAKIKA TANO NITAONDOKA KWENYE KAZI HII..
MKUU WA MKOA MOROGORO Dkt. Kebwe atangaza vita kwa wasiopeleka watoto shule
RC Kebwe Stephen Kebwe AZUNGUMZIA TAARIFA YA UGONJWA WA "DENGUE" Mkoani morogoro
CHUO CHA MZUMBE CHATOA MSAADA KWA MAJERUHI AJALI YA MOTO MOROGORO.
MKUU WA MKOA MOROGORO Dkt. Kebwe atangaza vita kwa wasiopeleka watoto shule
DKT. Kebwe awacharukia watendaji Ujenzi wa kituo cha Polisi kisaki
Mkuu wa Mkoa Morogoro Mhe.Dkt. kebwe atoa maagizo mazito .
Kiwanda cha Kwanza cha Kusafisha Dhahabu Kuanza Octoba Mwaka Huu.
TAZAMA Jinsi Rais Ramaphosa alivyo tembelea eneo la Mazimbu,Morogoro
Waziri Hasunga awahakikishia wakulima bei ya Mbolea haitopanda lazima ishuke

Wahisani

  • Wahisani